BOSI YANGA AFICHUA JAMBO KUHUSU USAJILI

BOSI wa Yanga kwenye idara ya Habari na Mawasiliano, Ali Kamwe amefichua jambo kuhusu usajili wa timu hiyo kuelekea msimu wa 2024/25.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua namna ilivyo kwenye suala la usajili hawana presha bali watafanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa.

Tayari Yanga ina uhakika kuendelea na Kocha Mkuu Miguel Gamondi baada ya kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja hivyo mbinu zake zitaendelea kutumika.

Kamwe amesema: “Tupo imara na tunatambua kwamba dirisha la usajili lipo wazi, hatuna presha katika hilo kikubwa ni kuwa na wachezaji wenye ubora na tunaamini itakuwa hivyo. “