AZAM YARIDHIA MAOMBI YA DUBE KUVUNJA MKATABA

Klabu ya Azam FC imeridhia maombi ya mshambuliaji wake Prince Dube ya kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ambayo aliyatoa mnamo mwezi Machi.

Taarifa ya Wanalambalamba hao imebainisha kuwa hatua hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo kutimiza matakwa ya kimkataba kama ilivyoainishwa kwenye vipengele vinavyoruhusu upande mmoja kuvunja mkataba.