LOMALISA HUYOOO NAMUNGO FC

BAADA ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili kwa mafanikio, Beki Joyce Lomalisa (31) anatajwa kutua Namungo FC kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Lomalisa awali alikuwa anatajwa kujiunga Simba lakini mambo yakaenda tofauti na sasa inaelezwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka miwili staa huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.