COASTAL UNION WANAWEZA WAKASHINDA KAMATI YA TFF ILA MBELE KUGUMU

Mgogoro wa Simba SC na Coastal Union kwa usajili wa Lameck Lawi kama umeufuatilia kwa makini kuna namna ambavyo mpaka sasa inaonyesha utaenda kumalizwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ama Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) tu. Ndiyo, CAF sio FIFA na FIFA sio CAS watu huwa wanachanganya hivi vyombo viwili, FIFA hawanaga Mahakama huwa wana Kamati/Bodi za maamuzi na CAS hawanaga Kamati au Bodi wenyewe ni Mahakama na hujishughulisha na michezo yote ilihali FIFA wao ni soka pekee.

Msikilize Cresentius Magori wa Simba SC halafu sikiliza viongozi wa Coastal Union, kisha fanya uchunguzi kidogo, halafu utagundua jambo moja kubwa kwamba Coastal Union walishauza mchezaji kwa Simba na walianza kupokea pesa kwa mafungu kwa ridhaa yao na makubaliano kwamba mpaka tarehe 31 MEI 2024 pesa ile imekamilika. Lakini mpaka tarehe 31 Mei walikuwa washapokea 170M kwenye akaunti yao na kubakia 35M ambayo ililipwa tarehe 10 Juni 2024 kufanya jumla ya 205M.

Tarehe za barua ya Coastal Union kwa Simba SC kuhusu kukiuka makubaliano kwa Simba SC zinakuonyesha kuna msukumo nyuma yake kiasi kufikia kujikanganya. Mwisho wa kulipwa ni tarehe 31 Mei, barua imeandikwa tarehe 14 Mei, siku 17 kabla ya kufikia tarehe ya makubaliano, walijuaje kwamba makubaliano yamekuukwa na tarehe haijafika? Tafsiri yake inaweza kuwa barua iliandikwa na ikawekwa tarehe ya nyuma, lakini kimaokosa huenda, katika harakati za kujiokoa na kinachoonekana sasa kitanzi cha Simba SC.

Uchunguzi wangu unasema kuna ofa ya Euro laki 300 (Tshs 848M) kutoka Ubelgiji ambazo Coastal Union watapata wakimuuza Lawi huko, wakati hapa wamepata 205M tu za “Kibongo”. Uchunguzi unapata nguvu na ukweli kwamba mpaka sasa Coastal wamesharejesha Tshs 205M zote ambazo Simba walilipa kwa mafungu, wao wamelipa mara moja tena kupitipitia bank ambako kuna ushahidi wa muda na tarehe, hii itawasumbua FIFA/CAS kama wanataka kumuuza mchezaji kweli, unavunja mkataba bila kutoa notisi ili umuuze tena, sijajua mshauri wao hapa alikuwa nani. Coastal walianza kupokea 20M kwa matumizi ya timu baada ya mkwamo,ligi ikiendelea, wamepata wapi hızı?

BİN KAZUMARI MTIPA