YANGA KAMBINI JULAI MOSI

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema kuwa maandalizi ya msimu ujao wa 2024/25 (Pre Season) kwa kikosi cha Yanga yataanza Julai Mosi.

Kupitia taarifa ya klabu hiyo imeelezwa kuwa kuhusu ni wapi kambi hiyo itawekwa na juu ya kikosi cha msimu huo kwa maana ya wachezaji wapya na walioachwa itajulikana wakati huo ambao timu hiyo itaingia kambini.