KAMPUNI na UBALOZI WASITISHA MKATABA na KIPANYA KISA TUHUMA za MWIJAKU – WAKILI AFICHUA HASARA KUBWA

Wanasheria wanaomwakilisha Masoud Kipanya, wamewaambia waandishi wa habari kwamba kwene barua walitomuandikia Mwijaku, walimueleza kuwa anatakiwa kumlipa mteja wao kiasi cha shilingi bilioni tano kama fidia kwa kumchafua na kutoa tuhuma za uongo dhidi yake.

Wakili Aloyce Komba kutoka kwa kampuni ya uwakili ya Haki Kwanza Advocates anayemwakilisha Kipanya kwa niaba ya mawakili wenzake, wamezungumza na waandishi wa habari na kueleza tuhuma alizozitoa Mwijaku na hatua walizozichukua mpaka sasa.

Mawakili hao wamesema wanalipeleka suala hilo mahakamani ambapo Mwijaku anatakiwa kuomba radhi, kumsafisha na kumlipa fidia ya shilingi bilioni 5 mteja wao.