AZIZ KI ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUENDELEA KUKIPIGA YANGA

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa kiungo wa Yanga SC, Stephan Aziz Ki amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga ndani ya Jangwani.

Nyota huyo amesaini mkataba huo hapo jana mbele ya wakala wake bwana Zambro Traore na rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said.

Kwa sasa nyota huyo anaelekea mapumzikoni na atarejea klabuni hapo Kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.