AZIZ Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga ujanja wake ndani ya uwanja ni mguu wa kushoto ambao ametumia kufunga mabao mengi zaidi.
Ipo wazi kuwa msimu wa 2023/24 nyota huyo ni namba moja kwa utupiaji akiwa katupia mabao 21 baada ya msimu kugota mwisho akiwa ni mfungaji bora.
Ujanja wake akiwa uwanjani ni kwenye mguu wa kushoto ambapo kafunga jumla ya mabao 17 akitumia mguu huo kuwaadhibu wapinzani.
Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi wakiwa namba moja kwenye msimamo na pointi zao ni 80.
Ki ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambapo alifunga bao moja kwa pigo la kichwa ilikuwa mchezo dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Mabao matatu kafunga kwa mguu wa kulia nyota huyo ambaye mkataba wake umegota mwisho msimu huu akiwa kwenye mazungumzo na mabosi wa Yanga kuongeza kandarasi nyingine.