UCHEBE WA SIMBA AULA SINGIDA BLACK STARS

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba SC Patrick Aussems ametambulishwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars SC kwa mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo msimu wa 2024/25.

Patrick Aussems alifahamika kwa utani jina la (UCHEBE) wakati anaitumikia klabu ya Simba na aliitumikia klabu ya Simba SC kuanzia mwaka 2018 hadi 2019.

Kwa maana hiyo ni wazi klabu ya Singida Black Stars wameachana rasmi na aliyekuwa kocha mkuu wao MECK MEXIME baada ya msimu kumalizika