SPORTPESA YATOA BONASI KWA YANGA MILIONI 537.5 KWA MAFANIKIO YA MSIMU ULIOMALIZIKA

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPESA ambayo ni Mdhamini Mkuu wa klabu ya Yanga imeikabidhi klabu hiyo mfano wa Hundi yenye thamani ya milioni 537.5 kama bonasi ya mafanikio ya klabu hiyo msimu uliomalizika.

“Leo tunakabidhi mfano wa Hundi kwa Klabu ya Young Africans SC kama BONUS ya mafanikio ya msimu. Hundi hii ina Thamani ya Tsh 537,500,000/= ambayo itawekwa kwenye akaunti za benki za Young Africans SC.” amesema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Sport Pesa, Mhe. Abbas Tarimba.

“Nawashukuru pia Wachezaji na benchi wa Young Africans SC kwa kile walichokifanya pale Zanzibar. Licha ya Wachezaji wetu wawili muhimu kukosa penati za mwanzo bado hawakupoteza malengo ya kuipambania nembo ya Klabu yetu ” Abbas Tarimba