KIUNGO HUYU YUPO HURU KUTUA BURE SIMBA AMA YANGA

BAADA ya msimu wa 2023/24 kugota mwisho timu zipo kwenye kusoma ripoti na kuangalia kipi ambacho watakifanya kuboresha timu zao kwa msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Tayari Azam FC wameanza kazi kwa kutambulisha nyota wapya ambao watakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2024/25 ambapo Azam FC na Yanga zitakuwa na kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuna mwamba kutoka Raja Club Athletic kwa sasa yupo huru hivyo kama mabosi wa Bongo iwe ni kutoka Simba ama Yanga wanahitaji saini yake watampata bure kwa kuwa ni mchezaji huru.

Yeye ni kiungo raia wa Afrika Kusini Haashim Domingo ana umri wa miaka 28 rekodi zinaonyesha kuwa amecheza jumla ya michezo 10 na ameanza kwenye michezo miwili pekee alitokea Mamelodi kama mchezaji huru.

Hivyo kama mabosi wa timu za Bongo watahitaji saini yake basi watampata bure kabisa kiungo huyo.