REAL MADRID YATHIBITISHA KUMSAINI MBAPPE

Baada ya kuachana rasmi na Klabu ya Paris Saint-Germain akiwa mchezaji huru, Kylian Mbappe (25) amejiunga na kikosi cha Real Madrid baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitano

Real Madrid imethibitisha kumsaini Mbappe ikiwa ni siku chache baada timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) kwa kuichapa Borussia Dortmund kwa Magoli 2-0

Taarifa zinaeleza mkataba huo unaenda sambamba na Mshahara wa takriban Pauni Milioni 12.8 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 42 kwa Mwaka, Tsh. Bilioni 3.5 kwa mwezi au Tsh. Milioni 875 kwa wiki