REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA ULAYA

REAL MADRID imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya KUMI NA TANO (15) kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi miamba ya Ujerumani, Borussia Dortmund kwenye fainali iliyopigwa katika dimba la Wembley, London.
Borussia Dortmund walikuwa bora sana kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuwaadhibu Mabingwa hao wa Uhispania kabla ya mambo kugeuka kichwa chini miguu juu kipindi cha pili pale Real Madrid ilipogeuka mbogo na kupata magoli mawili.
FT: Dortmund 🇩🇪 0-2 🇪🇸 Real Madrid
⚽ Carvajal 73’
⚽ Vini Jr 82’
Dortmund imekubali kipigo cha pili mfululizo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zote wakipoteza kwenye dimba la Wembley.
Itakumbukwa miaka 11 iliyopita Dortmund ilipoteza fainali dhidi ya Bayern Munich kwenye dimba la Wembley.