KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya betPawa imewazawadia vifaa vya michezo timu mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya soka na amsha amsha ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA kati ya Borussia Dortmund na Real Madrid itakayofanyika Jumamosi, Juni 1, 2024.
Tukio hilo lililopewa jina la Soka Live na betPawa litafanyika eneo la Kona ya Bwiru jijini Mwanza na lilipambwa na amsha amsha mbalimbali zikiwemo za mashindano madogo ya kandanda atakayoshirikisha klabu nne za eneo hilo.
Kabla ya mchuano huo, betPawa itatoa msaada wa vifaa vya mpira wa miguu kama jezi na mipira kwa timu ambazo ni Channel Africans FC, Bwiru FC, Majengo FC na Tiger FC.
“Tunaposubiri fainali ya kusisimua ya shindano la kifahari zaidi la Uropa, tunataka pia kurudisha kwa jamii zetu za mpira wa miguu na mashabiki kusaidia kujenga na kukuza michezo nchini Tanzania pia.” Amesema Meneja Masoko wa BetPawa Borah Ndanyungu.
“Mchezo huu una uwezo wa kutuletea heshima kama nchi na hakuna kinachozuia wanasoka wetu chipukizi kutamani kushiriki katika mashindano hayo mashuhuri,” amesema Ndanyungu.
Tukio la Soka Live na betPawa pia liliwahi kufanyika katika Mgahawa wa Juliana jijini Dar es Salaam Februari 11, 2024 wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Nigeria na Ivory Coast.
Katika hafla hiyo, wateja wa betPawa walishiriki challenge mbambali na kujishindia zawadi pamoja na burudani ya muziki mzuri, pamoja na kufurahia fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Kwa fainali ya mwisho ya UCL iliyofanyika Juni 10, 2023 mjini Istanbul, Uturuki, tukio la Soka Live la betPawa lilifanyika Dodoma, likiwakutanisha mamia ya mashabiki wa soka na usiku wa kufurahisha.