>

MTU WA KAZI ANASEPA YANGA

HUENDA mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakuwa ni wa mwisho kwa Joyce Lomalisa kuwa na uzi wa njano na kijani.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tabora United nyota huyo alitoq pasi moja ya bao kwa Aziz KI dakika ya 90 akiwa nje ya 18.

Yanga ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 leo watacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Azam Complex.

Miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakasepa Yanga ni pamoja na Skudu Makudubela, Okra Magic na Aziz KI.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe hivi karibuni aliweka wazi kuwa kuna wachezaji ambao wataondoka ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa kuna ofa ambazo zipo na wapo ambao watabaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa mazungumzo yanaendelea.

“Kuna wachezaji ambao mikataba yao inaisha hilo lipo wazi hivyo kikubwa ni kushubiri na kuona lakini muhimu Wanachama wa Yanga kuendelea kulipia kadi ili tupate fedha za kubaki na mchezaji ambaye tunamhitaji.”