DODOMA JIJI YAIPIGIA HESABU SIMBA

BENCHI la ufundi la Dodoma Jiji limebainisha kwamba limefanya maandalizi mazuri kukabiliana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ipo wazi kwamba mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka pointi tatu muhimu kutokana na nafasi ambazo timu hizo zipo.

Simba inapambana kujinasua kutoka nafasi ya tatu angalau ifike namba mbili huku Dodoma Jiji ikiwa na hesabu za kumaliza ndani ya 10 bora ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.

Kassim Lyogope kocha msaidizi wa Dodoma Jiji amesema kuwa wanatambua kwamba kazi kubwa ni kusaka ushindi mbele ya timu ya Simba.

“Kazi kubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba, tupo tayar kuwakabili na maandalizi muhimu yamefanyika kwa ajili ya kuona kwamba tunapata pointi tatu.”

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.