YANGA BALAA KWENYE UTUPIAJI HUKO

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Yanga ni balaa kwenye utupiaji wakiwa ni namba moja katika timu iliyofunga mabao mengi msimu wa 2023/24.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ni mabao 60 timu hiyo imefunga baada ya kucheza jumla ya mechi 27 ikibakiwa na mechi tatu kukamilisha mzunguko wa pili.

Kinara wa utupiaji ndani ya Yanga ni Aziz KI ambaye ametupia mabao 15 na pasi 8 za mabao kibindoni.

Namba mbili ni Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo timu hiyo imefunga jumla ya mabao 54 kibindoni kinara wa kutupia ni Feisal Salum akiwa na mabao 15.

Tatu ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ni mabao 51 safu ya ushambuliaji imefunga kwenye ligi ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo pia.

Licha ya Mtibwa Sugar kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja ni namba nne kwa timu yenye safu kali ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 27 ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi na pointi zake ni 20.