HIZI HAPA MECHI ZA LAKRED NDANI YA SIMBA

KIPA wa Simba, Ayoub Lakred rekodi zinaonyesha kwamba ni mechi 14 ameanza langoni msimu wa 2023/24 akiwa na uzi wa timu hiyo yenye maskani Msimbazi.

Kwenye mechi hizo amekomba dakika 1,260 akitunguliwa kwenye mechi 7 na hakutungiliwa kwenye mechi 7 pia ikiwa ni nusunusu ndani ya uwanja.

Ipo wazi kwamba kikosi cha Simba ndani ya tatu bora ni namba moja kwa timu iliyoruhusu mabao mengi ambayo ni 23 baada ya kucheza mechi 24.

Hizi hapa ni mechi za Lakred akiwa ndani ya Simba kwenye ligi pekee namna hii:-

Hizi hapa Simba haikufungwa ndani ya dakika 90-

1.Simba 3-0 Coastl Union

2.Simba 3-0 Kagera Sugar

3.Tabora United 0-4 Simba

4.JKT Tanzania 0-1 Simba

5.Simba 2-0 Mashujaa

6.Simba 2-0 Mtibwa Sugar

7.Simba 2-0 Tabora United

Hizi hapa Simba iliokota mabao nyavuni:-

Simba 1-1 Namungo

KMC 2-2 Simba

Simba 1-1 Azam FC

Coastal Union 1-2 Simba

Simba 3-1 Singida Fountain Gate

Yanga 2-1Simba

Namungo 2-2 Simba