MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga kituo kinachofuata ni dhidi ya Mashujaa ya Kigoma ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Yanga imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Kwenye mchezo wa CRDB Federation, Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United na katika mchezo huo kiungo Pacome Zouzoua ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti alipata nafasi yakucheza.
Mei 5 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa timu hizo mbili kupambania pointi tatu Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechu 24 inakutana na Mashujaa iliyo nafasi ya 14 na pointi 23.