MTIBWA SUGAR HAINA HOFU NA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex, Mei 3 2024.

Ipo wazi kwamba mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Manungu ulisoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba hivyo Mtibwa wanapambana kulipa kisasi na Simba wanapambana kulinda rekodi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Simba wataingia kwa tahadhari zote.

“Hatuna hofu na mchezo wetu dhidi ya Simba, tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu imara na tunatambua kwamba imetoka kucheza mashindano ya kimataifa hilo halitupi hofu zaidi ya kufanya maandalizi mazuri.

“Wachezaji wapo tayari na tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo wenye ushindani mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu muhimu,”.