FUNGAFUNGA MICHEL FRED AWAIBUA SIMBA

MWAMBA Michel Fred ambaye Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba anapenda kumuita fungafunga ameweka wazi kuwa mashabiki waendelee kuwa na mshikamano mambo mazuri yanakuja.

Timu hiyo imetinga hatua ya fainali Kombe la Muungano 2024 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ inatarajiwa kumenyana na Azam FC Aprili 27 katika mchezo wa fainali.

Ipo wazi kwamba mfungaji wa kwanza Muungano 2024 ni Fred ambapo alifanya hivyo katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza.

Nyota huyo amesema: “Tuna kazi kubwa ya kufanya wachezaji hivyo mashabiki ni muhimu kuwa pamoja nasi kwenye mechi ambazo tunacheza kikubwa ni kuwa pamoja,”.

Kwa upande wa Ally ameandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa Instagram: “Wakati mwingine Matokeo yasiyoridhisha ya timu huwa yanafifisha ubora wa mchezaji mmoja mmoja au matokeo mazuri ya timu hua yanaficha madhaifu ya mchezaji mmoja mmoja.

“Fredy Michael Fungafunga tangu amewasili Simba Sports amefunga jumla ya Magoli 10 katika mashindano yote aliyoshiriki ni wastani mzuri sana kwa mshambuliaji.

“Champions league 1, Ligi kuu ya NBC 4, Kombe la Crdb 4, Kombe la Muungano 1.

“Imani yangu ni kwamba kadri anavyopata muda wa kucheza, kadri anavyoaminiwa ndivyo anathibitisha ubora wake.

“Kwetu sisi Wana Simba jukumu letu ni kumuunga mkono Mshambuliaji wetu na tukumbuke ya kwamba hii ndio nafasi ngumu zaidi kwenye mpira duniani kote

“Kwa alichokionesha Fredy hatuna budi kusimama nae ili atufikishe kwenye kilele cha mafanikio,”