AZAM FC KUIKABILI KMKM MUUNGANO

KLABU ya  Azam FC matajiri wa Dar wanakibarua kigumu kwenye mchezo wa nusu fainali Muungano 2024 dhidi ya KMKM kwa kila mmoja kusaka ushindi kusonga mbele hatua ya fainali.

Ikumbukwe kwamba Aprili 24 Simba ilikuwa na kibarua mbele ya KVZ na iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo imetinga hatua ya fainali ikisubiri mshindi wa leo kukutana naye kwenye hatua ya fainali.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Ni Aprili 22 matajiri hao wa Dar waliwasili Zanzibar kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 huku timu zote zikipiga hesabu kupata ushindi kwenye mchezo huo na kutinga hatua ya fainali.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema: “Maandalizi ambayo tumefanya ni mazuri ni suala la kusubiri muda wa mchezo tupate kutoa burudani kwenye mchezo wetu ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, tupo tayari na muda ni sasa kwa ajili ya kupata ushindi,”.