SIMBA KWENYE KAZI LEO MUUNGANO

SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Kombe la Muungano dhidi yaKVZ ambao unatarajiwa kuchezwa leo Aprili 24, Uwanja wa New Amaan Complex.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na kazi dakika 90 kusaka matokeo ambapo kwenye mechi zake tano mfululizo kimekwama kupata ushindi.

Matola amesema; “Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu na wapinzaniwetu sio timu ya kubeza tupo tayari kupata matokeo mazuri.

“Kuwa kwenye mashindano haya ni jambo kubwa na tunafurahi kwa kuwa haya mashindano yalikuwepo miaka 20 iliyopita na sasa yamerejea, wachezaji wapo tayari na tuna amini tutapata matokeo mazuri,”.

Mchezo huu ni nusu fainali kwa kuwa kuna timu nne ambapo KMKM itakuwa dhidi ya Azam FC, Aprili 25 2024.

Miongoni mwa nyota wa Simba waliopo Zanzibar ni pamoja na Pa Omary Jobe, Israel Mwenda, Ally Salim, Clatous Chama.