Skip to content
KIKOSI cha Simba leo kimeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Muungano Cup 2024.
Simba haijawa kwenye mwendo mzuri ndani ya ligi baada ya kukwama kuonyesha uwezo wake wa kutumia nafasi dhidi ya Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara.
Mzunguko wa kwanza ilipoteza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.
Mzunguko wa pili ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba hivyo ndani ya dakika 180 Simba ilikwama kukomba pointi mbele ya Yanga iliyokomba pointi sita.
Timu mbili kutoka Tanzania zitashiriki mashindano hayo ikiwa ni pamoja na Azam FC ambao wao waliwasili Zanzibar Aprili 22.
Mashindano haya ambayo yanatarajiwa kuanza leo Aprili 23 yamerejea kwa mara nyingine baada ya kupita miaka 20.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Pa Omary Jobe, Babacar Sarr, Che Malone.