MATAJIRI wa Dar, Azam FC wametia timu ndani ya Lindi ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Jumapili, Aprili 14 2024.
Ikumbukwe kwamba kweye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Namungo walikomba pointi tatu mazima.
Hivyo mchezo wa mzunguko wa pili Azam FC wanawafuata Namungo wakiwa na hesabu za kulipa kisasi huku Namungo wakiwa na hesabu za kulinda ushindi wao.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 21 inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 9 na pointi 23 baada ya kucheza mechi 21.
Mapema Aprili 12 2024 msafara wa Azam FC uliwasili Ruangwa na kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao ujao.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amebainisha kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao dhidi ya Namungo.