MSAFARA wa Yanga ukiwa na jumla ya wachezaji 26 miongoni mwao akiwemo Mudhathir Yahya, Jonas Mkude, Clement Mzize, Pacome, Yao umewasili salama nchini Afrika Kusini.
Timu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imepokelewa na balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwanà.
Aprili 5 2024 Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wa mkondo wa pili Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ule uliochezwa Machi 30 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns.