>

SIMBA INAHITAJI WASHAMBULIAJI WA KAZI, KOCHA ATUMA UJUMBE

PENGINE mbinu ya kuanza bila ya mshambuliaji halisi kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ilitokana na washambuliaji waliopo ikiwa ni Michael Fred na Pa Jobe kushindwa kufikia matakwa ya Kocha.

Kocha huyo wakati anaanza majukumu ndani ya Simba aliweka wazi kuwa hakuna mwenye uhakika namba kikosi cha kwanza ndio maana kuna nyakati Clatous Chama mbali na kutokuwa na nidhamu alikuwa anaanzia benchi.

Ikiwa Simba ina malengo yakufika mbali kimataifa inapaswa kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi na kutambua kwamba kuwatoa Al Ahly nchini Misri asitafutwe mchawi wakati inajulikana mchawi ndugu.

Baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly, Abdelhak Benchikha aliweka wazi kuwa wanahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa licha ya wachezaji wake kujituma.

“Unaona kwenye mchezo wetu tumepoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly lakini wao kwenye benchi walikuwa bado na wachezaji wenye uwezo hivyo nasi tuna kazi ya kuwa kwenye ubora,”.