SIMBA WANA KAZI KUMALIZA KWA MKAPA, UGENINI BALAA

IKIWA Simba itakosa ushindi mbele ya Al Ahly angalau mabào manne Uwanja wa Mkapa inakwenda kuwa ngumu kwa sababu Al Ahly wakiwa Uwanja wa taifa wa Cairo wanashambulia kama nyuki.

Katika mchezo wa African Football League uliochezwa Misri Oktoba 24 2023 ubao ukasoma Al Ahly 1-1 Simba walicheza mpira wa kasi mwanzo mwisho.

Ni mashuti 20 walipiga kuelekea lango la Simba huku mawili yakilenga lango sawa na Simba lakini Simba walipiga mashuti 8 pekee kueleea lango la Al Ahly.

Al Ahly walikuwa kwenye mtego wa kuotea mara 9 na Simba mara 2 hii inamaana kwamba Al Ahly wakiwa nyumbani hawajui suala la kupaki basi wao wanakuja mwanzo mwisho.

Simba wanakazi ngumu Uwanja wa Mkapa, Machi 29 kumaliza kazi inawezekana ikiwa wachezaji watakuwa na utulivu kwa kupunguza makosa kwenye eneo lao na kutumia makosa ya wapinzani.

Abdelahk Benchikha, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa wanakutana na timu kubwa na yenye uzoefu hivyo wanahitaji kuwa makini zaidi.