
LIGI YA MABINGWA AFRIKA: SIMBA 0-1 AL AHLY
KUPOTEZA kwa Simba kwenye robo fainali ya kwanza Uwanja wa Mkapa kunaongeza ugumu kwa timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali. Wachezaji wa Simba watajilaumu wenyewe kuwa kwenye mwendelezo wa kukwama kutumia nafasi ambazo walizitengeneza ndani ya dakika 90. Haijaisha mpaka iishe kazi itakuwa kwa Yanga Machi 30 kufunga mchezo wa hatua ya robo fainali…