SIMBA YAKAMILISHA KAMBI SASA KAMILI KUWAVAA AL AHLY

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wamewasili Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Kikosi cha Simba Machi 19 kiliweka kambi Zanzibar kwa ajili ya kambi maalumu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 29 ambao ni hatua ya robo fainali.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye kambi hiyo ni pamoja na mshambuliaji Fred MichaelPa Jobe, Henock Inonga, Shomari Kapombe, Che Malone.

Kapombe ameweka wazi kuwa wachezaji wote wanatambua kazi kubwa iliyopo kwenye kusaka ushindi dhidi ya Al Ahly hivyo watashirikiana kupata matokeo mazuri.

“Kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo wetu dhidi ya Al Ahly pamoja na ugumu uliopo, nina amini kwamba tutashirikiana kupata matokeo chanya kwenye mchezo