KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Machi 29 2024 Uwanja wa Mkapa Legend Saleh Ally ameweka wazi kuwa Simba wanapaswa kuwa makini kuelekea mchezo huo wasiwachukulie pia wapinzani wao kwa kuwa Al Ahly ni moja ya timu imara ambazo zinajua namna ya kufanya kwenye hatua za mtoano kimataifa