VAR KUTUMIKA RASMI KATIKA MECHI ZA LIGI KUU BARA KUANZIA MSIMU UJAO
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema vifaa vya kiteknolojia kwa ajili ya kuwasaidia waamuzi (VAR), vitaanza kutumika rasmi katika mechi za Ligi Kuu Bara kuanzia msimu ujao. Karia pia amekaribisha maoni ya kanuni ya kuzikata timu pointi ambazo wachezaji au mashabiki wake wataonekana kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina na kuingia uwanjani wakati…