MWAMBA Prince Dube anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba ambao wanahitaji kuipata saini yake kwa ajili ya kuiboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Ikumbukwe kwamba ikiwa Simba watapata saini ya nyota hiyo kuna wachezaji watakaopewa mkono wa asante kwenye upande wa ushambuliaji.