MACHI 16 Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea ambapo kutakuwa na dakika 90 za jasho kwa wanaume kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
Saa 10:00 jioni, Singida Fountain Gate watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba wakiwakaribisha Namungo FC
Singida Fountain Gate na Namungo wanakutana ikiwa wote wametoka kupoteza michezo yao iliyopita.
Namungo Machi 8 mchezo wake wa mzunguko wa pili wa ligi ilikuwa dhidi ya Yanga baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 1-3 Yanga.
Pointi tatu zikiwa ni mali ya Yanga inayofundishwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Singida Fountain Gate kwenye mchezo wao uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Simba 3-1 Singida Fountain Gate.
Kwenye mchezo huo Thomas Ulimwengu alipachika bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.