Pambano la mwisho kati ya Pep Guardiola na Jurgen Klopp kwenye Ligi Kuu England limemalizika kwa sare ya 1-1 katika dimba la Anfield.
FT: Liverpool 1-1 Manchester City
⚽ Mac Allister (P) 50’
⚽ John Stones 23
Hili ni pambano la 30 kati ya Klopp na Pep Guardiola ambapo Mjerumani huyo ameshinda mara 12, Mhispania akishinda mara 11 huku mechi 7 zikimalizika kwa sare.
Liverpool imefikisha alama 64 sawa na kinara Arsenal na wanasalia nafasi ya pili huku Manchester City wakifikisha alama 63 na wanasalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.