KLABU ya Arsenal imeweka rekodi mpya ya kufunga mabao mengi zaidi ndani ya Ligi Kuu England katika mechi saba mfululizo.
Arsenal imefunga mabao 31 na kuipiku rekodi ya Man City iliyowekwa msimu wa 2017/18 ambapo ilifunga mabao 28.
Arsenal pia imeandika rekodi mpya ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya kushinda kwa mabao 5+ kwenye mechi tatu mfululizo za ugenini.
Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta mchezo wake uliochezwa Machi 4 2024 ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mkubwa.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Sheffield United 0-6 Arsenal ambayo kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu na pointi 61 huku vinara wakiwa ni Liverpool wenye pointi 63 wote wamecheza mechi 27.