YANGA KUMALIZA VINARA WA KUNDI KIMATAIFA

ANAANDIKA Jembe

Yanga wana nafasi kubwa ya kuongoza kundi kama watakuwa makini na kuamua kukusanya pointi Cairo.

Ahly si Belouizdad na Ahly si wepesi hasa wakiwa Cairo lakini Yanga kwenda Cairo wakiwa wamefuzu inaweza ikawa.

FAIDA…Wakijipanga na kuichukulia mechi kwa umakini zaidi

HASARA…Kama wataichukulia kwa wepesi sababu walishinda kabla Vs Belouizdad

Kushinda nafasi ya kwanza kwenye kundi kuna faida ya kukaa port number one kwenye upangaji wa robo fainali.

Ikumbukwe kwamba tayari kikosi cha Yanga kipo Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuchezwa Machi Mosi 2024.

Kwenye kundi D Yanga imekusanya pointi 8 baada ya kucheza mechi tano na vinara Al Ahly wao wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 9.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Al Ahly ambapo bao la Yanga lilifungwa na Pacome.