YANGA KUWAFUATA WAARABU WA MISRI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AL Ahly ya Msiri unaotarajiwa kuchezwa Machi Mosi 2024 huku wakiwa kamili gado kuwafuata wapinzani wao kwenye mchezo huo.

Ali Kamwe ambaye alipata changamoto ya kiafya muda mfupi baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanakwenda wakiwa kamili kutafuta ushindi.

“Timu inatarajia kuondoka saa 11:55 jioni kuelekea Misri, tutaondoka na shirika la ndege la Ethiopia na kufika saa 2:33 usiku, kisha tutaondoka Ethiopia na kuwasili Cairo saa saba usiku kuamkia kesho. Timu itafikia Royal Kempinski Hotel.

Tutaondoka na msafara wa watu 60, msafara huu umegawanyika makundi matatu, wachezaji 24, benchi la ufundi 13, na Watendaji/maofisa wakuu wa klabu 23 hii ni muhimu kwetu kwenda kuendelea burudani kwa mashabiki.

“Niwapongeze wachezaji kwa kupambana na jitihada zao zikaenda kuzalisha furaha kwa mashabiki, jasho lao limekwenda kutengeneza rekodi kuwa klabu ya kwanza kushinda mabao 4 dhidi ya timu kutoka ukanda wa kaskazini hususani taifa la kiarabu tena bingwa wa ligi.

“Nitakuwa mkosefu wa fadhila kwa kushindwa kuwashukuru benchi letu la ufundi chini ya Miguel Gamondi, wameandaa wachezaji vizuri, kiakili na kimwili. Unaongelea CR Belouizdad ambaye amecheza dakika 180 bila kuruhusu kufungwa, na kufanikiwa kuwauzia Al Ahly kushindwa kulenga hata shuti moja. Kimsingi kama wachezaji wasingeandaliwa vizuri basi isingekuwa shughuli nyepesi, : amesema Kamwe