Home Sports SIMBA YATANGAZA VIINGILIO MECHI YA JUMAMOSI DHIDI YA JWANENG KWA MKAPA

SIMBA YATANGAZA VIINGILIO MECHI YA JUMAMOSI DHIDI YA JWANENG KWA MKAPA

“Tarehe 2 ya mwezi wa tatu tunakwenda kushinda tena ushindi wa kihistoria na kwenda robo fainali. Jwaneng tunamheshimu lakini amekuja wakati mbaya.”

“Tiketi zimeshaanza kuuzwa na niwakumbushe Wanasimba rekodi zote ambazo tuliziweka, ziliwekwa na Wanasimba wenyewe. Wakati tunamfunga AS Vita mara 2, wakati tunamfunga Horoya mabao 7 ushindi wote ulitokana na mashabiki wa Simba. Ili tumnyoe Jwaneng tunawahitaji Wanasimba.”

“Viingilio ni;
Mzunguko – Tsh. 5,000
VIP C – Tsh. 10,000
VIP B – Tsh. 20,000
VIP A – Tsh. 30,000.”

“Kuna tiketi za Platinum kwa Tsh. 150,000. Utapata kifurushi maalumu kutoka Simba, usafiri kutoka hotelini hadi uwanjani ukiwa na escort pamoja na chakula.”

“Tumeongeza kifurushi kingine kinaitwa Tanzanite, hii anayenunua anakaa pale VVIP, kama akija Infantino au Mhe. Rais Samia unakaa nae eneo moja. Hii inauzwa Tsh. 200,000. Unapata car gate pass, chakula na vinywaji. Watu wa Tanzanite na Platinum wapige simu 0742771311.”

“Vilevile tuna Mnyama Package, watu kuanzia 20 ambao watanunua tiketi kwa pamoja watapewa car gate pass na kukaa sehemu moja wakiwa uwnajani. Lakini pia tuna Executive Tickets hii ni kwa ajili ya makapuni au mashirika, tutawapa na car gate pass.”

“Tangu jana tiketi zinapatikana na nitoe rai kwa Wanasimba wanunue tiketi haraka iwezekanavyo. Mechi hii tunataka mashabiki waujaze Uwanja wa Mkapa, mechi hii ni muhimu na ni jukumu la kila Mwanasimba kuipeleka Simba robo fainali. Njoeni wote Simba ni yetu sote. Watu 60,000 tunawahitaji.”

“Maumivu ya Oktoba 24, 2021 hakuna Mwanasimba ambaye ameyasahau na hakuna ambaye atasahau, Jwaneng Galaxy walitusababishia maumivu haya. Asante Mungu muda umefika wa kwenda kufuta haya maumivu.”

“Vita ya kisasi kila mtu anatakiwa kutumia silaha yake, Mwanasimba mwenye silaha yoyote, dua yoyote afanye tukamfanye vibaya Jwaneng Galaxy. Tukishinda tutakuwa na faida tatu, moja kuingia robo fainali, ya pili kulipa kisasi na ya tatu kuingia kwenye historia kuingia robo fainali mara nne mfululizo.”- Ahmed Ally.

Previous articleAHMED ALLY AMSHANGAA KAMWE KUZIMIA KISA GOLI 4 – ”SIMBA TUSHAMFUNGA MTU GOLI 7”…
Next articleSIMBA YAPANIA KUWAFUNGA JWANENG KUTINGA ROBO FAINALI