YULEYULE shujaa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji, Mudathir Yahya leo tena kafunga bao la ushindi dhidi ya Mashujaa.
Dakika ya 85 zikiwa zimesalia dakika tano mpira kugota mwisho akafunga bao la ushindi na kuipa pointi tatu Yanga inayofikisha pointi 37 ikiwa namba moja kwenye msimamo.
Kipindi cha pili Mashujaa wamepata bao la kuweka usawa dakika ya 65 kupitia kwa Mtumbuka ambaye amefunga bao hilo akiwa ndani ya 18.
Kipindi cha kwanza Maxi Nzengeli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mashujaa linamfanya afikishe mabao 8 kibindoni.
Iliwabidi Yanga wasubiri mpaka dakika ya 44 kupata bao hilo la kuongoza kwenye mchezo wa ligi katika dakika 45 za kipindi cha mwanzo.
Maxi sasa anaachana na namba ya jezi yake rasmi Februari 8 mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Azam Complex kwa kuwa awali alikuwa na mabao 7.