WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza maalumu la waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini “TASWA Media Day Bonanza 2024”.
Bonanza hilo maalumu linatarajiwa kufanyika Februari 10, 2024 Msasani Beach Club, Dar.
Tukio hilo linatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, litahusisha pia uzinduzi wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2024, zinazotolewa na TASWA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TASWA, tukio hilo litahusisha mchezo wa riadha, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, kushindana kunywa soda, kushindana kufukuza kuku na kushindana kula ugali na kuku mzima wa kuchoma.