MUDA MKALI WA MABAO YA USIKU YANGA

KWENYE mechi ngumu ambazo wapinzani wa Yanga walikuwa wakicheza kwa kujilinda zaidi, kiungo Mudathir Yahya alikuwa ni mkali wa kutibua mipango hiyo na kuipa timu hiyo pointi tatu mazima Uwanja wa Azam Complex.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilipata sare yake ya kwanza msimu wa 2023/23 Februari 2 ubao wa Uwanja wa Kaitaba uliposoma Kagera Sugar 0-0 Yanga ambapo wapinzani wao walitumia mbinu ya kujilinda zaidi.

Ngoma ilikuwa nzito Februari 5 baada ya dakika 85 za kucheza bila kufungwa, Dodoma Jiji walishuhudia bao la jioni likifungwa na Mudathir dakika ya 86 akitumia pasi ya Nickson Kibabage.

Ipo wazi kwamba wakali wote hao wawili walianzia benchi, Mudathir aliingia dakika ya 61 akichukua nafasi ya Jonas Mkude na Kibabage aliingia dakika ya 76 akichukua nafasi ya Joyce Lomalisa.

Mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na Mudathir kutibua mipango kwa bao la usiku ilikuwa dhidi ya Namungo, ilikuwa ni Septemba 20 2023 alipofunga bao dakika ya 87.

Bao hilo alilofunga kiungo huyo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo ilikuwa ni zama za Cedrick Kaze ndani ya Namungo FC.