UONGOZI wa Tabora United umesema kuwa hauna hofo na mchezo wao dhidi ya Simba ambao utakuwa wa ligi wapo tayari kuchukua pointi tatu kwa namna yoyte watakapokutana ndani ya uwanja.
Ofisa Habari wa Tabora United, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi walichonachopamoja na usajili mzuri waliofanya unawapa nguvu ya kupata matokeo kwenye mechi zao zote watakazocheza.
Timu hiyo inafundishwa na Kocha Mkuu Guran Kuponovic ambaye anawapa mbinu wachezaji wa timu hiyo inayopambana kufanya vizuri katika mechi za ligi na mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
βTunawakaribisha Simba watakuwa ugenini kwenye mchezo wetu ujao hatuna hofu ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu.
Haiishi mpaka iwe imekwisha na wachezaji wetu wana rekodi nzuri ikiwa ni pamoja na mlinda mlango John Noble ambaye amecheza mechi 12 na hajafungwa kwenye mechi tano.
βSio ulinzi langoni pekee bali mpaka eneo la ushambuliaji wanfanya vizuri ikiwa ni pamoja na Eric Okutu amecheza mechi 11 na kuhusika katika mabao matano, katoa pasi moja ya bao na kufunga mabao manne hivyo tuna wachezaji wazuri tunaamini tutapa ushindi kwenye mchezo wetu ujao,β.