>

SIMBA 4-0 TEMBO RAUNDI YA PILI

KIPINDI cha pili Simba imefunga mabao mawili na kukamilisha dakika 90 kwa ushindi wa mabao 4-0.

Mabao ya kipindi cha pili yamefugwa na Karabaka pamoja na Jobe ambapo wote walitokea benchi kwenye mchezo wa leo.

UBAO wa Uwanja wa Azam Complex mchezo wa raundi ya pili Kombe la Azam Sports Federation mshambuliaji mpya wa Simba ameanza kikosi cha kwanza.

Ni Michael Fred ambaye ni mshambuliaji anayepewa nafasi ya kubeba mikoba ya Jean Baleke aliyekutana na thank you.

Dakika 45 za mwanzo ubao unasoma Simba 2-0 Tembo ya Tabora huku mabao yakifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 31 na Luis dakika ya 11.

Langoni ni Hussein Abel ameanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo huku beki Kennedy Juma akiwa beki kiongozi kwenye ukabaji.