YANGA baada ya kucheza mechi 11 za Ligi Kuu Bara imeambulia ushindi kwenye mechi 10 ikipoteza mchezo mmoja ikiwa haijapata sare ndani ya msimu wa 2023/24.
Timu hiyo ina balaa kutokana na kasi yao kuwa imara ndani ya ligi wakiwa wanatetea taji hilo ambalo walitwaa msimu wa 2022/23.
Kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambaye alichukua mikoba ya Nasreddine Nabi aliyekuwa akiwanoa wachezaji hao.
Kwenye upande wa utupiaji namba moja ni kiungo mshambuliaji Aziz KI ambaye katupia mabao 10 kibindoni sawa na namba ya jezi ambayo anavaa mgongoni akiwa na uzi wa Yanga.
Jumla safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 31 na mfungaji wa bao la kwanza ni beki wa kupanda na kushuka Dickson Job ilikuwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya KMC.
Gamondi amesema kuwa malengo makubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ni kupata matokeo mazuri na kuwa kwenye malengo yao.
“Tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa hivyo nasi tunafanya kazi kubwa kuwa imara kwa ajili ya mechi za kitaifa na kimataifa,”.