KAZI IMEPAMBA MOTO AFCON

NIGERIA wamewafungashia virago Cameroon katika 16 bora Kombe la Mataifa Afrika kwa ushindi wa mabao 2-0 kazi ikizidi kupamba moto kwa kila timu kupambania ushindi.

Ni balaa zito kwenye mashindano haya ambapo Tanzania yenye Mbwana Samatta, Kibu Dennis, Mzamiru Yassin, Dickson Job, Bacca iligotea hatua ya makundi na kuondolewa ikiwa na pointi mbili kibindoni.

Kwenye mchezo huo wa kibabe ni  dakika ya 36 Ademola Lookman alifungua pazia la mabao na kamba nyingine tena ilikuwa dakika ya 90. Hivyo Nigeria hao robo fainali.

Angola wao wamepenya hatua ya 16 bora mpaka robo fainali baada ya ushindi wa mabao 3-0 Namibia katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Mabao ya Angola yalifungwa na Gelson Dala dakika ya 39, 42 alitupia mabao mawili na moja ni mali ya Agostinho Mabululu dakika ya 67.