REKODI HIZI HAPA ZA JEMBE JIPYA SIMBA

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Simba ambaye ni mshambuliaji rekodi zake zinaonekana kumbeba ikiwa zitajibu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Tayari nyota huyo ambaye ni mshambuliaji Michel Fredy ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake ndani ya Simba kwa ajili ya mechi za kitaifa na kimataifa.

Rekodi zinaonyeshwa kwamba raia huyo Ivory Coast aliyekuwa kwenye majukumu yake ndani ya Green Eagles katika mechi 18 alifunga jumla ya mabao 14 akiwa na pasi nne za mabao.

Baleke anasepa ndani ya Simba akiwa kafunga mabao 16 ndani ya ligi kuanzia msimu wa 2022/23-23/24 alipofunga mabao nane kila msimu na mpaka anakutana na asante alikuwa ni kinara wa utupiaji akiwa nayo 8 kibindoni.

Ahmed Ally meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua uimara wa wachezaji waliopo ndani ya Simba watawapa furaha.