MUDA WA KUFANYA KWELI NI SASA KILA KONA
KAZI kubwa ambayo inapaswa kufanyika kuelekea kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa ni kufanya kweli kwa kila timu kupata matokeo mazuri. Tumeona kwamba kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) Tanzania ilikwama kutinga hatua ya 16 bora na kuishia kwenye hatua za makundi. Kwa maana hiyo kuna makosa ambayo wachezaji waliyaona na kushindwa kuyatumia…