SIMBA KUREJEA KAZINI

KIKOSI cha Simba leo Januari 25 kinatarajiwa kurejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za kitaifa na kimataifa.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu,Abdelhak Benchikha ilitoka kushiriki Mapinduzi 2024.

Kwenye mashindano hayo iliishia nafasi ya pili na bingwa akiwa ni Mlandege.

Januari 13 2024 ilikuwa ni fainali na ubao ulisoma Mlandege 1-0 Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na mpango mkubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.

Tunatambua ushindani ni mkubwa na tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mechi zijazo.

“Mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi tunaamini tutafanya vizuri na inawezekana,”.