JUMA Mgunda, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa wamejifunza mengi baada ya kugotea hatua ya makundi katika Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON).
Katika mechi tatu Stars ilipoteza mchezo mmoja dhidi ya Morocco inayoongoza kundi F ikiambulia Sare mbili dhidi ya Zambia 1-1 Tanzania na Tanzania 0-0 DR Congo mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia Januari 25.
Mgunda amesema kwa hatua ambayo wamefika wanamshukuru Mungu wanaamini wakati ujao watarejea wakiwa imara.
“Tunamshukuru Mungu kwa yote na katika mashindano haya tumejifunza mengi wakati ujao tutarejea tukiwa imara. Pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wamejituma katika kutimiza majukumu yao,”.